Mshambuliaji wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta amepaa usiku wa kumkia leo kuelekea Ubelgiji kukamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Kuondoka kwa Samatta ni kama kunamaliza sintofahamu iliyogubika hatima ya wapi atakapoelekea baada ya mkataba wake na Mazembe kumalizika, huku mmiliki wa timu hiyo akiweka ngumu kumruhusu kujiunga na Genk akitaka aende Ufaransa kwenye klabu ya Nantes.
Safari ya Samatta kuelekea Ubelgiji, imethibitishwa na familia yake ambayo imelazimika kuahirisha sherehe iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza.
Baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Ally Samatta alisema sherehe hiyo ambayo ilikuwa ifanyike leo, haitokuwapo kutokana na safari ya Mbwana kwenda Ubelgiji.
“Sherehe haitafanyika kesho (leo), kwani Samatta anaondoka usiku wa leo (jana) kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na Genk ya Ubelgiji na sisi kama familia tumepanga kuifanya siku nyingine,” alisema
Mwananchi
0 comments:
Chapisha Maoni