MASHABIKI wa Mbeya City wameanzisha staili mpya kabisa ya ushangiliaji huku wakiimba nyimbo za kuwatia moyo wachezaji wao wakiwa uwanjani, japo nyimbo hizo zinaacha maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka kutokana na aina ya maneno wanayotumia, taarifa hii imenukuliwa na Fichuo kutoka gazeti la Mwanaspoti.
Juzi Jumamosi City ilijitupa uwanjani kuikabili Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na walifanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 10.
Mashabiki hao ambao hawakuwa wengi tofauti na ilivyozoeleka zamani, wakiishangilia timu yao, walionekana kucheza kwa staili mbalimbali, huku wakiimba nyimbo ambazo maneno yake yalikuwa tata.
“Leo tunataka goli, ushindi ni lazima...Masela komaeni hatuna baba wala mama... Masela komaeni..’.
Kwa muda ule mashabiki wengi ambao hawakuwa sehemu ya waimbaji hao walionekana kujiuliza juu ya mistari ya ‘Masela komaeni hatuna baba wala mama masela komaeni’, ndipo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo Mwanaspoti liliamua kuwafuata mashabiki hao na kuwauliza walikuwa wakimaanisha nini.
Mmoja wa mashabiki hao, Juliana Haule alisema wanaimba nyimbo hizo ili kuwatia moyo wachezaji wao kwani hivi sasa timu hiyo inaonekana kuchukiwa na viongozi kuanzia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Chama Cha Soka Mkoa wa Mbeya (Mrefa) na wengine kutoka serikalini ndio maana wanaamua kupaza sauti zao kuwaambia wachezaji kwamba ni lazima ‘wajiongeze wenyewe wasitegemee msaada wowote’.
Alisema City imekuwa ikifanyiwa vurugu na mambo mengine ya hujuma ambayo ni ya wazi wazi, lakini
viongozi wamekuwa wakiziba masikio na macho jambo wanaliona kama vile uwepo wa timu hiyo katikaLigi
Kuu hakuwafuharishi wengi.
“Mwaka jana tulienda Tanga kucheza na Coastal, tulifanyiwa vurugu na wachezaji kupigwa mawe, lakini
hakuna hatua zozote hadi leo zilizochukuliwa, kama hiyo haitoshi mchezaji wetu Juma Nyoso kafungiwa
katika hujuma tupu,” shabiki mmoja alisema.
Shabiki mwingine, Bad Boy alisema: “Tumeshajijua kwamba timu ipo kwenye mpango wa kuhujumiwa.”
0 comments:
Chapisha Maoni