Mwanamume mkongwe zaidi duniani amefariki nchini Japan akiwa na umri wa miaka 112.
Yasutaro Koide, kutoka jiji la Nagoya, alizaliwa tarehe 13 Machi 1903 na alifanya kazi kama fundi wa nguo wakati wa ujana wake.
Alitambuliwa na Guiness Book of World Records kama mwanamume mzee zaidi duniani Agosti mwaka jana.
Alipoulizwa kuhusu siri ya maisha marefu alipokuwa hai, anadaiwa kuwashauri watu waache kujiumiza sana na kazi na pia waishi kwa furaha.
Bado haijabainika ni nani atamrithi kama mwanamume mzee zaidi aliye hai duniani.
Kwa sasa mtu mkongwe zaidi duniani ni Mwamerika, Susannah Mushatt Jones, ambaye ana umri wa miaka 116.
Alichukua nafasi hiyo mwaka jana baada ya kifo cha Misao Okawa kutoka Japan aliyekuwa na umri wa miaka 117.
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997.
0 comments:
Chapisha Maoni