Kama ulikuwa ukisikia tetesi kila kona kwamba Klabu ya Soka ya Arsenal
ya England ilikuwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji kutoka
FC Basel ya Uswisi, Mohamed Elneny, basi jua kwamba hiyo si tetesi tena
bali ni ‘cofirmed’.
Akizungumza na waandishi wa habari mpaka stori hiyo kuifikia Umbeya
Umbeyani, kocha Arsene Wenger amesema kuwa dili la mchezaji huyo
limekamilika kwa kutoa kitita cha paundi milioni 5 (zaidi ya bilioni 10)
na hivyo kuna uwezekano wa kucheza mechi ya Jumapili dhidi ya Stoke
City.
“Tunafurahi kumuona amejiunga na sisi, natumaini atakuwepo katika mechi
dhidi ya Stoke City siku ya Jumapili,” alisema Wenger baada ya mechi
dhidi ya Liverpool iliyomalizika kwa mabao 3-3
Mbali na habari hiyo, pia ile iliyo chini ya kapeti inasema kwamba
mchezaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez anaweza kuwepo hiyo Jumapili baada
ya kukosa mechi kadhaa sababu ya kuwa majeruhi.
0 comments:
Chapisha Maoni