Mwigizaji na mwanamitindo wa nchini Marekani, Karrueche Tran jana
jioni alinaswa akidendeka na mpenzi wake wa kike Christina Milian katika
Klabu ya The Nice Guy iliyopo magharibi mwa Hollywood nchini Marekani.
Warembo hao waliweka wazi mahusiano yao mwaka jana baada ya Karrueche
kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Chris Brown huku
Christina akiwa tayari amembwaga mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Lil
Wayne.
Mbali na mahusiano hayo, lakini inaonyesha Karrueche mwenye umri wa
miaka 27 bado anapambana na changamoto za maisha ya mapenzi ya jinsia
moja kitendo kilichopelekea jana aandike katika ukurasa wake wa Twitter
kuwa kwa sasa amefungua milango ya mahusiano mapya na kwamba yupo tayari
kumpokea mpenzi baada ya kukaa mpweke kwa muda mrefu japo alidai
itakuwa vigumu kumpata mpenzi wa kweli ambaye ataweza kumpa penzi ya
dhati.
0 comments:
Chapisha Maoni