Mkurugenzi wa
makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza amkabidhi jezi Rais wa TFF, Mh Jamal
Malinzi kwaajili ya michuano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama
Taifa Women Cup ambayo yanatarajiwa kutimua Vumbi tarehe 1 Januari 2015 huku
Mechi ya Uzinduzi ikiwakutanisha timu kutoka Mwanza na Musoma mechi ambayo
itapigwa katika Dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
Kampuni ya
Proin Ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya ambayo yanatarijiwa kutimua Vumbi
Mnamo tarehe 1 Januari 2015. Proin Imeamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo
la Kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake ambapo baadae wachezaji bora
wataweza kuingia katika Timu ya Taifa ya Wanawake.
Vilevile Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mh Jamal Malinzi amewataka pia
makampuni mengine Kujitokeza katika Kudhamini Mashindano haya yanayotarajiwa
kuanza tarehe 1 Januari 2015 kwa lengo la Kuweza kuinua vipaji vya Mpira wa
Miguu kwa Wanawake huku pia wakipata fursa ya Kujitangaza kibiashara kwasababu
mpira wa miguu ni mchezo ambao unapendwa sana na watu wengi hivyo ni dhahiri
kabisa Kuwa Makampuni mengi yakidhamini mashindano haya yataweza kufikia
malengo yao kwa kujitangaza.
0 comments:
Chapisha Maoni