Jumatatu, Oktoba 20, 2014

ZIARA YA CHADEMA IRINGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na ziara yake ya nchi nzima kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuisoma na kuipitia kwa makini katiba inayopendekezwa kisha kupiga kura ya ndio au hapana pindi mda utakapowadia.
Akihutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa katika viwanja vya stendi ya Mlandege Manispaa na Mkoa wa Iringa katibu wa Chadema Kitaifa Dkt.Wilbroad Slaa amesema katiba ndio msingi wa maendeleo ya nchi yetu katika nyanza zote hivyo wananchi wana haki ya kuikataa au kuikubali katiba inayopendekezwa kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na miaka hamsini ijayo.
Dkt.Slaa ameongeza kuwa kadri siku zinavyoenda ndivyo kutakuwa na mikutato mingi itakatoyofanywa na vyama mbalimbali vya siasa hivyo wakazi wa Mkoa wa Iringa wawe makini na zoezi la upigaji kura ya ndio au hapana kwa kutoshinikizwa na makundi ya watu hasa viongozi wa vyama vya siasa.
Aidha amewataka wananchi kujiaandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ambalo huandikishwa na viongozi wa kata husika pamoja na kushiriki zoezi la upigaji kura siku za uchaguzi ili kuwapata viongozi wenye nia ya kuwaletea maendeleo.
Pia Dkt. Slaa amesema Chama cha Chadema kikiwa ni chama cha upinzani wanaendelea na mazungumzo na vyama vingine vya upinzani vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ili waweze kukubaliana na kufikia muafaka wa kumsimamisha mgombea mmoja mmoja katika chaguzi zote zijazo.
Licha ya mkutano huo kuwa na lengo kuu la kutoa elimu kwa wananchi juu ya katiba inayopendekezwa kwa upande wa Mbunge wa jimbo la Manispaa ya Iringa Mch.Peter Msigwa ametoa tathmini ya maendeleo ya sekta mbalimbali kuanzia kipindi cha 2010-2014 ambapo amewaasa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii pia serikali kuendelea na maboresho na ukarabati wa miundo mbalimbali hasa barabara na vituo vya afya.
Hata hivyo Mkutano huo ambao umefanyika october 19 mwaka umehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu kutoka visiwani Zanzibar Salum Mwalimu na viongozi ngazi mbalimbali wa Chadema Manispaa ya Iringa.

0 comments:

Chapisha Maoni