Jumatano, Oktoba 29, 2014

TSH. 400000 ZAUA MTU MBEYA

Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina wala makazi yake mara moja, umri kati ya miaka 25 – 30, jinsi ya kiume ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kuchomwa moto na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kukutwa akiwa amevunja nyumba ya Hussein Hashim (22) Tanyboy na kuiba tshs 400,000/=.
Tukio hilo limetokea janausiku wa saa 04:00 katika mtaa wa viwandani, kata ya Mwakibete, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa mhanga baada ya kumuona mtuhumiwa alipiga kelele za kuomba msaada na wananchi kujitokeza na kumshambulia marehemu.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

0 comments:

Chapisha Maoni