Jumatano, Oktoba 29, 2014

TANESCO IRINGA VITANI NA VISHOKA

Shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Iringa limewataka wananchi kutowatumia mafundi bandia maarufu kama‭ ‬vishoka ili kuepukana na kutapeliwa kwa huduma zitolewazo na shirika hilo.
Kaimu‭ ‬ meneja TANESCO mkoa wa Iringa Mhandisi Seraphine Lyimo‭ ‬amesema mafundi bandia hupelekea wananchi kuunguliwa nyumba na vifaa vingine kutokana na kuunganishiwa nyaya bila utaratibu.
Mhandisi Lyimo‭ a‬mesema‭  mafundi bandia hushiriki kuiba ‬umeme hali ambayo inalikosesha mapato ya  shirika hilo hivyo kuchelewesha maendeleo ya mkoa kiuchumi.
Aidha, amesema Shirika la ugavi wa umeme linaendelea na msako wa watu wanaotoa huduma za shirika hilo kinyume na sheria ili wafikishwe kwenye vyombo husika kwa ajili ya hatua za kisheria.
Hata hivyo, kaimu meneja wa TANESCO mkoa wa Iringa ameshauri wananchi kutoa taarifa pindi wanapowaona watu wanaoiba umeme ili kuondokana na majanga ya moto ambayo husabisha vifo na madhara mengine.

0 comments:

Chapisha Maoni