KATIKA MSAKO WA KWANZA,
Mtu mmoja aitwaye Albert Laison (31) mkazi wa Lualaje anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya akiwa na bhangi nusu debe.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 25.10.2014 majira ya saa 09:00 asubuhi huko katika kitongoji cha Kabuta, kijiji cha Lualaje, kata ya Lualaje, tarafa ya Kipembawe, wilaya ya chunya, mkoa wa Mbeya katika msako uliofanyika maeneo hayo.

Mtuhumiwa ni muuzaji wa bhangi hiyo, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
AIDHA, KATIKA MSAKO WA PILI,
AIDHA, KATIKA MSAKO WA PILI,
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mashaka Ally (19) mkazi wa Chimala anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya akiwa na bhangi debe moja na nusu.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 25.10.2014 majira ya saa 13:20 mchana huko Check Point – Inyala, kata ya Inyala, tarafa ya Tembela, wilaya ya Mbalizi, mkoa wa Mbeya.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 25.10.2014 majira ya saa 13:20 mchana huko Check Point – Inyala, kata ya Inyala, tarafa ya Tembela, wilaya ya Mbalizi, mkoa wa Mbeya.
Mtuhumiwa alikutwa na bhangi hiyo aliyokuwa ameiweka kwenye mfuko wa Sulphate akiwa anaisafirisha kutoka Chimala kwenda Mbeya mjini kwa mauzo.
Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi hiyo, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
KATIKA MSAKO WA TATU,
KATIKA MSAKO WA TATU,
Watu watu waliofahamika kwa majina ya 1. Julius Chuwalo (56) 2. Edina Charles (44) na 3. Eva Msokwa (40) wote wakazi wa Mlowo wakiwa na pombe ya moshi ujazo wa lita 30 na mtambo mmoja wa kutengenezea pombe hiyo haramu.
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 25.10.2014 majira ya saa 08:00 katika msako uliofanyika huko katika kijiji cha Mlowo, kata ya Mlowo, tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa ni wauzaji wa pombe hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya na pombe haramu ya moshi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

Aidha, anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za mtu/watu au mtandao wa watu wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji wa bidhaa haramu ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
0 comments:
Chapisha Maoni