Jumatatu, Oktoba 27, 2014

ALICHOZUNGUMZA PADREW NEWCASTLE UNITED

Meneja wa klabu ya Alan Pardew amewatahadharisha mashabiki wa klabu hiyo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki ambacho inaonekana mambo yameanza kuwaendea vyema baada ya msoto wa miezi miwili iliyopita.

Pardew, amesema si wakati mzuri kwa mashabiki wa Newcastle United, kuanza kumwagia sifa kutokana na matokeo yanayooekana viwanjani, zaidi ya kuendelea kuwa pamoja na kikosi chao kwa kukipa nguvu kila kinapocheza nyumbani ama ugenini.
Amesema alikuwa katika wakati mgumu na mara kadhaa aliwasisitiza mashabiki kuwa wavumilivu na kumpa muda wa kufanya mabadiliko ya uchezaji kwenye kikosi cha The Magpies, hivi anaona bado kuna ulazima wa kaliba hiyo kuendelea.
Ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Spurs uliopatiakana jana unakua wa pili mfululizo kwa klabu hiyo ya St James Park, ambapo hali hiyo imeanza kuwarejesha mashabiki kwenye mipango ya kuanza kumuamini Pardew.
Kabla ya ushindi dhidi ya Spurs Newcastle Utd waliifunga Crystal Palace bao moja kwa sifuri ikiwa ni baada ya matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Swansea City.
Kufuatia matokeo hayo Newcastle Utd wamechupa hadi katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na point 10.

0 comments:

Chapisha Maoni