Jumanne, Oktoba 28, 2014

MATOKEO YA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA IRINGA

Watoto zaidi elfu arobaini na watu wazima elfu sabini wa manispaa ya Iringa Mkoa wa Iringa wamepata chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella.
Mratibu wa chanjo Manispaa ya Iringa Bibi Bertha Lyimo amesema, zoezi hilo limefanikiwa kutokana na wananchi kutambua umuhimu wa afya zao.
Bibi Lyimo amesema watoto ambao hawajapata chanjo hiyo wapo kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya utindio wa ubongo na  upofu wa macho.
Aidha amesema watu wazima hawajapata chanjo hiyo kwa kiwango kizuri kutokana na kutokuwa na vituo vya kudumu vya kutolea chanjo hiyo.
Hata hivyo,  mratibu wa chanjo manispaa ya Iringa amewataka watu wazima ambao hawajapata chanjo ya Rubella kutembelea vituo vya afya kupata chanjo hiyo ili kuepukana na maradhi ya kiafya.  

0 comments:

Chapisha Maoni