Jumatatu, Oktoba 27, 2014

KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA IRINGA

Wananchi wa Mkoa wa Iringa wameaswa kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Dec 14,mwaka huu kwa kuchagua kiongozi atakaye kuwa chachu ya maendeleo ya mtaahusika.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Bw.Miraji Mtatulu ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa stendi ya Mlandege Manispaa ya Iringa.
Bw.Mtatulu ameongeza kuwa ili mtaa na kata husika iwe na maendeleo viongozi wa vyama vya siasa hawana budi kuziondoa tofauti za uvyama wao pindi chaguzi zinapoisha na matokeo kutangazwa kwa wananchi.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bi.Jesca Msambatavangu amesema katika kuelekea kipindi cha kuipigia kura ya ndio au hapana katiba  iliyopendekezwa,wananchi wametakiwa kuwa makini na matamko yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.
Hata hivyo,kiasi cha shilingi milioni moja kimetolewa na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa kwenye vituo vya mashina mapya ya vijana likiwepo la stendi ya Mlandege kama mtaji wa kuanzisha kazi za ujasilia mali ili waweze kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana.

0 comments:

Chapisha Maoni