Ijumaa, Septemba 12, 2014

WAWILI WAKAMATWA NA GONGO MBEYA

Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili, Jane Andembwise mwenye miaka 41 anayeishi Uyole na Jackson Mlungu aliye na miaka 58 mkazi wa Itezi hapa mkoani Mbeya baada ya kukutwa na pombe haramu ya moshi (Gongo) lita moja na nusu.
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako uliofanyika jana saa nne asubuhi  katika eneo la Uyole, kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga jiji na mkoa wa Mbeya na imefahamika kuwa watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa pombe hiyo, taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
Pamoja na hayo kamanda wa polisi wa Mbeya Ahmed Msangi ameithibitishia Fichuo Tz juu ya kutukia kwa tukio hilo na kutoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe hiyo haramu ya moshi maarufu kama gongo kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari pia kwa afya.

0 comments:

Chapisha Maoni