Umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba wasichana zaidi
ya milioni 120 duniani kote,sawa na msichana mmoja kati ya kumi atakua
amaebakwa ama amewahi kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
kabla hajatimiza umri wa miaka 20.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia
masuala ya watoto UNICEF kimegundua mnamo mwaka 2012 pekee watoto na
mabinti wapatao elfu tisini na watano waliuawa,wengi wao ni kutoka
Marekani kusini na Caribbean.
Ripoti hiyo ya UNICEF iliangazia nchi zipatazo
mia moja na tisini, na kusema kwamba duniani kote watoto wametendewa
ukatili,mauaji na mashambulizi ya kingono ikiwemo kuonewa na uadabishaji
watoto unaokiuka haki zao.




0 comments:
Chapisha Maoni