Alhamisi, Septemba 11, 2014

WATANZANIA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI LEO SEPTEMBER 11

Leo dunia inakumbuka tukio kubwa na baya la kigaidi lilolofanywa na kundi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama Bin Laden mwaka 2001 baada ya kushambulia majengo ya kitengo cha ulinzi cha Marekani jijini Washington na jengo la biashara huko New York na kuuawa takribani watu 3,000.
Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia vitendo vya kigaidi vinavyozidi kushamiri katika ukanda wa Afrika hususani kundi la Alshabaab linalofanya mashambulizi ya kushitukiza katika nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamesemwa na mnadhimu wa kikosi cha usalama barabarani (SACP), Johansen Kahatano.
Kahatano ameeleza kuwa hivi sasa kundi la Alshabaab lipo katika harakati ya kulipiza kisasi kufuatia kuuawa kwa kiongozi wao na majeshi ya Marekani hivyo raia wanapaswa kuwa makini na kutoa taarifa mara moja polisi pale wanapomtilia mashaka mtu yeyote.
Nitoe wito tu kwa wananchi kwamba tuchukue tahadhari ya kutosha sisi wenyewe kwa maana ya kutaka kujilinda dhidi ya jamii inayotuzunguka. Unapokuwa na mashaka na mtu ambaye hafahamiki sawasawa, awe amebeka kitu ambacho kinatia shaka. Hasa kwenye mabasi pale unamuona mtu anasafiri na mzigo wake halafu anashuka anauacha pale kwenye basi. Hata katika mikusanyiko ya watu wengi, ukishakuwa na mashaka na mtu lazima taarifa itolewe kwa askari.
Ameeleza.

0 comments:

Chapisha Maoni