Jumanne, Septemba 09, 2014

WANAFUNZI 21540 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA IRINGA

Jumla ya wanafunzi 21540 mkoani Iringa wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kuanzia Septemba 10 hadi 12 mwaka huu.
Afia elimu wa Mkoa wa Iringa Bw. Joseph Mnyikamba amesema kati ya watahiniwa hao wavulana ni 9779 na wasichana 11761 ambapo idadi hiyo imepungua kutoka 23149 mwaka jana. Bw. Mnyikamba amesema maandalizi mtihani huo yamekamilika ikiwemo kupeleka vifaa vyote kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Iringa.
Aidha Afisa elimu wa mkoa amewashauri wazazi kuwahimiza watoto wao kwenda kufanya mitihani huku akiwaasa wanafunzi kuzingatia maelekezo wanayopewa na wasimamiza wao.
Wakati huo huo Afisa Elimu wa Manispaa ya Iringa Bw. Halfani Masukira amesema zaidi ya Wanafunzi 3000 kutoka shule 49 za Manispaa ya Iringa wakiwemo wasichana 1689 na wavulana 1575 wanatarajia kufanya mtihani huo.
Bw. Masukira amesema watahiniwa 336 watafaya mtihani huo kwa lugha ya kiingereza wakati 2909 watatumia lugha ya kiswahili na wanafunzi 11wenye ulemavu wa kusikia na 8 wenye uono hafifu ambapo watafanya mtihani wao maalum.
Hata hivyo, Afisa elimu wa mkoa Bw. Mnyikamba amewakumbusha wanafunzi na walimu kuepuka udangannyifu katika mitihani ili kuepuka kufutiwa mtihani na walimu kufukuzwa kazi.

0 comments:

Chapisha Maoni