Ben McMahon kutoka Melbourne, Australia, hawezi
kukmbuka kuwa alikuwa hali mahututi alipohusika na ajali ya barabarani
zaidi ya wiki moja iliyopita, lakini alichokikumbuka alipoamuka kutoka
katika hali yake kinastaajabisha. McMahon aliamka kutoka katika usingizi mzito yaani , 'Coma,' akiwa na uwezo wa kuzungumza kichina.
Wazazi
wake walikuwa na furaha isiyo na kifani kupata taarifa za mwanao kuwa
bukheri wa afya, lakini walipigwa na mshangao kugundua uwezo wake kwa
kuzungumza lugha mpya. McMahon alijifunza lahaja ya Mandarin akiwa shuleni , lakini ana kiri kuwa hakuwa na uwezo wa kuongea kichina.
Kwa
siku zake za kwanza baada ya kutoka katika hali yake mahututi, McMahon
angeweza tu kuzungumza na kuandika Mandarin. Ilimchukua muda kuanza
kuweza kuongea kiingereza ambayo ndiyo lugha yake ya kwanza. Hata baada ya kuanza kuzungumza kiingereza tena, uwezo wake wa kuongea Mandarin ulisalia.
Hii
leo McMahon anatumia uwezo wake mpya wa kuongea lugha hiyo kwani
anaishi na kusomea Shanghai, na pia ametumia muda wake kuwaelekeza
watalii kutoka China na hata kuwa na kipindi cha kichina kwenye
televisheni.
Daktari aliyemtibu McMahon amestaajabishwa na uwezo
wake kuongea kichina na hata kuelezea kilichojitokeza katika mgonjwa
wake kama jambo la kipekee ambalo limezua mjadala tayari.
Hata
hivyo anasema kuwa sehemu ya ubongo wa McMahon iliyomsaidia kuongea
kiingereza iliharibiwa katika ajali na kufanya sehemu ya akili yake
iliyokuwa na ufahamu mdogo kuhusu kichina kuanza kutumika.
Vyovyote madakatri wanavyoka kuieleza hali hiyo,McMahon ana furaha ya kuendelea kuzungumza lugha mbili tofauti kwa sasa.




0 comments:
Chapisha Maoni