Jumatano, Septemba 10, 2014

USHAURI WA DULLY SYKES KWA DIAMOND NA ALIKIBA

Nyota wa zamani wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amewataka wakali wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ na Ally Kiba, watoe ‘Collabo’ ili kukusanya mashabiki wa muziki huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Dully alisema, kwa hali ya kawaida watoto wa kiume hawawezi wakawa na mabifu yasiyoisha kama watoto wakike.
Diamond na Ally Kiba wanatakiwa kutoa collabo ili sisi mashabiki wao tukubali kwamba hawana ugomvi, watoto wa kiume kuwekeana mabifu sio vizuri, wimbo ambao wataimba pamoja najua itakuwa moto wa kuotea mbali
alisema Dully.
Hivi karibuni, vyombo mbalimbali vya habari vililipoti ugomvi wa wasanii hao ambao unatokana na kila mmoja kujiona ni bora zaidi kuliko mwenzie.
Dully ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri kupitia kazi zao kutokana na kujitahidi kutunga mashairi yenye ubora ambayo yanawavutia wapenzi wake.

0 comments:

Chapisha Maoni