Jumatano, Septemba 10, 2014

JOHN BOCCO NJE AZAM FC

Captain John Bocco pamoja na jana kufanya mazoezi katika Gym ya kisasa pale Chamazi - Azam Complex, lakini vipimo alivofanyiwa mchana na mtaalamu (physiotherapist) Gilbert Kigade pale Msasani Peninsula Hospital ili kuangalia maendeleo yake, alibainisha kwamba Bocco anatakiwa apumzike kwa wiki 3 huku akipata matibabu. Bocco anasumbuliwa na maumivu ya misuli na hivyo ataikosa mechi ya Jumapaili dhidi ya Yanga na pia michezo 3 ya mwanzo ya Ligi kuu ya Vodacom.

0 comments:

Chapisha Maoni