Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya nchini, Godfrey Nzowa
amesema mawasiliano baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
yamefanikisha kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
Akizungumza na Fichuo Tz, Nzowa ambaye pia
ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) alisema wanafanyakazi
kama timu kwa nchi za Afrika Mashariki na duniani kuhakikisha wanaweka
mipango madhubuti ya kudhibiti uingizaji na uuzaji wa dawa hizo.
Akitoa mfano, alisema katika kipindi hiki ni vigumu kwa wauzaji
kupata hata kilo moja hivyo wanalazimika kutafuta kwa gharama kubwa
zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni