MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), kitengo cha Ushuru na Forodha, leo wanatarajiwa kuanza kutoa huduma ya kuvushwa mizigo katika mpaka Tunduma kwa kutumia mfumo mpya ujulikanao kwa jina la (TANCIS), badala ya ule wa zamani (SYCUDA).
Kwa mujibu wa Meneja wa Mamlaka hiyo Mkoa wa Mbeya, Anold Mahimu, mfumo huo utaanza kufanya kazi katika ofisi za mamlaka hiyo kitengo cha ushuru na forodha na kwamba, hata mawakala wanapaswa kutoa huduma kwa njia hiyo mpya kutokana na kuwa mfumo huo ni wa kimtandao na pia unapunguza mzunguko.
Katika hatua nyingine, Meneja huyo alisema kuwa ni wajibu kwa mawakala kukabiliana na changamoto zitakazo kuwa zikijitokeza wakati huu wa kuanza kwa mfumo huo, licha ya kuwa ni wa uwazi kuliko mfumo wa awali.
Alisema kumekuwa na tabia katika jamii kuwa na mivutano isiyo ya lazima, hasa inapotokea mfumo mpya unaanza kufanya kazi na kwamba, si vema kukata tamaa bali ni wajibu kwa wadau kukabiliania nao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mawakala walioshiriki mafunzo kuhusiana na mfumo huo mpya, Renatus Rwezaura, alisema mafunzo hayo yalikuwa mazuri na kwamba, mfumo huo umepunguza usumbufu ambao wamekuwa wakipata wa kupita kila ofisi kwa ajili ya kupitisha taarifa mbalimbali za mzigo, lakini kwa sasa shughuli zote zinaweza kufanyika ofisini kwa njia ya mtandao.
Mafunzo hayo yalishirikisha baadhi ya watumishi kutoka idara mbalimbali zinazoshirikiana na TRA ambazo ni Polisi, Uhamiaji, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mifugo na Uvuvi pamoja na mimea na chakula.

0 comments:
Chapisha Maoni