Alhamisi, Septemba 04, 2014

SHERIA MPYA ZA VAN GAAL KUHUSU CHAI NA MATUMIZI YA SIMU KWA WACHEZAJI MAN U

Kila mtu huwa na utaratibu wake katika kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa, kuwa na sheria binafsi katika mambo yako ni kujitengenezea wepesi wa kufikia malengo yako katika jambo lolote maishani. Hata katika mchezo wa soka pia huwa hivyo, mbali na zile sheria 17 za soka uwanjani, baadhi ya sheria binafsi za kocha huwa ni kati ya mambo yanayochangia maendeleo mazuri ya timu husika kama ilivyo kwa kocha mpya wa Manchester United, Louis Van Gaal.
Yeye Van Gaal kwa sasa kajiwekea sheria zake ili kuweka nidhamu kwa wachezaji wake, sasa wachezaji wa Manchester United wanalazimika kukabidhi simu zao usiku kabla ya mechi yoyote.
Mbali na sheria hiyo pia kocha huyo ameweka sheria nyingine inayomtaka kila mchezaji yeyote kuwahi chai ya asubuhi siku ya mchezo na kama sivyo basi mchezaji atakayekwenda kinyme na maagizo hayo hatomtumia katika mchezo huo.

0 comments:

Chapisha Maoni