Mahakama Kuu nchini Tanzania leo imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa
na raia kupinga kuendelea kwa Bunge la Katiba linalokutana huko Dodoma.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na jopo la majaji watatu inasikilizwa
katika wakati ambapo bado kunaendelea kushuhudiwa malumbano makali baina
ya wabunge walioko bungeni na kundi la UKAWA ambalo limesusia bunge
hilo kwa madai ya kupindishwa kwa baadhi ya vipengele vilivyowasiliwa
kwenye rasimu ya katibu.



0 comments:
Chapisha Maoni