Jumatatu, Septemba 01, 2014

MAUAJI IRINGA

Si picha halisi
Watu wanne wamefariki Mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwepo la watu watatu kuuawa kwa tuhuma za imani ya kishirikina huku jeshi la polisi likiwashikilia watu kumi kwa kuhusika na mauaji hayo.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhan Mungi amesema Elioti Mlasi umri miaka 60,Martini Lung’alika umri miaka 51 na Yamulisi Ngandago umri miaka 78 wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Itimbo wilaya Kilolo Mkoani Iringa wamefariki baada ya kupigwa kwa fimbo sehemu mbalimbali za miili yao kwa tuhuma za Imani ya kishirikina.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa kutokana na mauaji hayo jeshi la polisi linawashikilia watu kumi kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo ambapo majina yao yamehifadhiwa kwa sababu maalumu za kiuchunguzi.
Wakati huo huo Kamanda amesema Severa Msoliwoya umri miaka 29 mkazi wa kijiji cha Mdete wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa amefariki baada ya kukatwa kwa panga sehemu ya mkono wa kushoto na mme wake Linus Ng’owo.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa ambapo jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ambaye amekimbia baada ya kutekeleza mauaji hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni