Uongozi wa klabu ya Man Utd umeripoti kupata hasara kubwa ya
kipato chake cha kila mwaka licha ya kuonesha faida nzuri wakati wa
uongozi wa David Moyes kama maneja.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ya nchini Uingereza,
imeeleza kuwa kipato chake cha kila mwaka kilishuka kwa asilimia 84,
ilihali faida yake iliongezeka kwa zaidi ya asilimia ishirini.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake
mjini Manchester unatarajia kipato chake cha mwaka 2015 kushuka zaidi,
kutokana na matokeo mabovu yanayoendelea kuwaandama, hasa kwenye
michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza, ambapo hatua hiyo
inajitokeza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Aidha, taarifa hiyo imeonyesha wazi kwamba, wakati wa meneja David
Moyes na jopo lake walipata jumla ya Dola milioni nane kama malipo ya
kuachishwa kazi mapema mwaka huu baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha
miezi zaidi ya sita.
0 comments:
Chapisha Maoni