Alhamisi, Septemba 11, 2014

MAJAMBAZI YAVAMIA BAR NA GUEST HOUSE MBEYA KISHA KUJERUHI NA KUPORA MAMILIONI

Majambazi 6 wakiwa na silaha wamevamia katika Bar na nyumba ya kulala wageni mkoani Mbeya katika wilaya ya Momba  mijini Tunduma iitwayo Feel Happy huku wakiwa na silaha aina ya Short Gun (Bunduki) na kujeruhi kisha kupora pesa nyingi usiku wa kuamkia leo.
Maafisa wa jeshi la polisi mkoani Mbeya wakizungumza na Fichuo Tz Blog mkoani Mbeya wamesema kuwa mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo amefaham,ika kwa jina la Simon Enock mwenye miaka 42 ambaye ni mkazi wa Namtambalale ambapo amejeruhiwa katika mguu wake wa kulia na kuvunjika kabisa.
Aidha majambazi hayo yamepora kiasi cha shilingi 1,800,000/=.
Pamoja na tukio hilo lililotokea katika nyumba ya kulala wageni, pia usiku huo huo majambazi hayo yalipora pesa ambazo zilikuwa ni mauzo ya siku nzima katika Bar ambazo mpaka sasa haijafahamika kuwa ilikuwa ni kiasi gani.
Mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo amelazwa katika kituo cha afya Tunduma akiendelea kupatiwa matibabu huku baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamebainika na msako mkali wa kuwatafuta walio salia ukiendelea kwa kushirikiana na askari wa nchini Zambia kwani baada ya tukio hilo walikimbilia Chianga nchini Zambia.

0 comments:

Chapisha Maoni