Jumatano, Septemba 03, 2014

JESHI LA POLISI TANZANIA MASHAKANI KWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema Jeshi la Polisi limekuwa likitumia nguvu kubwa katika kuwashughulikia watuhumiwa wa kesi mbalimbali nchini.
Pia imesema nguvu, ambayo imekuwa ikitumika kuwashughulikia watuhumiwa ni pamoja na kuwatesa, kuwadhalilisha, kuwabambikia kesi, kuwekwa kuzuizini kwa muda mrefu, bila kufikishwa mahakamani pamoja na mazingira magumu ya dhamana jambo linalokiuka haki za binadamu.

0 comments:

Chapisha Maoni