Mario Balotelli ndio kwanza amerejea England,
kwa mara ya pili, lakini inaonekana haijamchukua muda mrefu kuhit katika
vichwa vya habari, safari hii kwa kuonesha "ladha" ya mitindo na mambo
anayopenda.
Mchezaji huyo wa Liverpool aliyenunuliwa kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16, amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya mji, - eneo la Helsby, Cheshire - na kufanya ndio "keja".

Na kama picha
hizi pamoja na habari ambazo zimeandikwa na magazeti na tovuti kadhaa
hapa Uingereza ni za kuaminika, basi inaonekana Balotelli ameonesha
'staili' yake kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani yake ni pauni
milioni 4.7.
Nyumba hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja na kila kitu ambacho mchezaji soka , Kijana, milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama bwawa la kuogelea, sauna, chumba cha kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya kutua helikopta, uwanja wa mpira.. Na vingine 'vidogovidogo'.

0 comments:
Chapisha Maoni