Alhamisi, Septemba 04, 2014

ANDY MURRAY ATOLEWA US OPEN

Nyota wa tennis raia wa Scotland, Andy Murray ameondolewa katika mashindano ya US Open kwa kipigo cha seti 3-1 kutoka kwa Mserbia Novak Djokovic kwenye hatua ya robo fainali.
Murray alipoteza pambano hilo kwa seti 7-6, 6-7, 6-2, 6-4 mbali na kiwango kizuri alichoonyesha.
Kwa ushindi huo, Djokovic atakwaana na Mjapan, Kei Nishikori katika nusu fainali ya michuano hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni