Alhamisi, Agosti 28, 2014

UMBO NA SURA VILINIPAGAWISHA, KUMBE NYUMA YAKE...

Habari zenu... Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana! Mwaka jana mwezi wa tatu nilifunga ndoa na mke wangu. Tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume. Kitu kikubwa kilichosababisha nikamuoa ni sura yake ya kuvutia, sauti yake tamu pamoja na umbile lake kwa ujumla. Kiukweli ameumbika sana. Tatizo alilo nalo mke wangu ni kwamba kwa sasa hakamatiki! Hatulii. Anatembea hadi na marafiki zangu. Kibaya zaidi ni kwamba siku hizi kila nikitaka kufanya naye mapenzi ananiambia hajisikii kufanya hivyo. Ameanza kunidharau na kuniona mimi sina hadhi kwake. Inaniuma sana. Wazazi wa pande zote mbili wamejaribu kulitatua hili bila mafanikio. Sasa nimeona kabla ya kuchukua maamuzi mengine mazito nimeamua niwashirikishe mnipe ushauri wenu. Nisaidieni kuokoa ndoa yangu jamani.

0 comments:

Chapisha Maoni