Alhamisi, Agosti 28, 2014

8 MBARONI KWA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA MBEYA

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 08 kwa kosa la kunywa pombe kabla ya muda. Watuhumiwa hao ni pamoja na 1. Jafet Sambwe, 2. Lucas Mwakapemba (21) mkazi wa Ilemi 3. David Mwaipopo (23) mkazi wa Sinde 4. Ezia Lazaro (24) mkazi wa Manga 5. Esau Mwandenga (25) mkazi wa Sangu 6. Tamika Bukuku (27) mkazi wa Ilolo 7. Victoria Mahamudu (25) mkazi wa Sangu na 8. Rosta Mwakilembe (34) mkazi wa Jua Kali.
Watuhumiwa walikamatwa jana majira ya saa 04:45 asubuhi huko maeneo ya stand kuu, Ilolo Sinde na Ikete, kata na tarafa ya Sisimba, jiji na mkoa wa Mbeya. Taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anawataka wananchi kutii sheria bila shuruti kwani unywaji wa pombe kabla ya muda ni kinyume cha sheria.


0 comments:

Chapisha Maoni