Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Alli Omari
Juma amefuta matumaini ya Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba mpya,
badala yake akabainisha kuwa wajumbe wako Dodoma kwa ajili ya kula posho
tu.
Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa ni mambo ya kulazimishana kila upande, sisi wengine tunaona bora ya Ukawa waliotoka nje kuliko mambo ya humu ndanialisema Juma na kuongeza:
..Hata wale Wapemba waliokwenda Umoja wa Mataifa kudai haki ya kujitenga , naona walikuwa halali kwani hapa bungeni hakuna mwakilishi hata mmoja kutoka huko wakati tunaambiwa kuwa itakuwa Katiba ya wote, ni kudanganyana.
Mjumbe huyo alisema kuwa Rasimu ya Warioba
imetupwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuwafanya wengine
waone kuwa kinachotengenezwa ni marekebisho ya Katiba ya 1977.
Alisema kuwa suala la akidi pia litakuwa ni moja
ya vikwazo vitakavyosababisha kutopatikana kwa Katiba, akitolea mfano
kutoka kwenye kamati yake Namba 4.
Alisema ndani ya kamati hiyo mambo mengi yanachakachuliwa kwani wajumbe wanaotakiwa kutoka Zanzibar ni 14 lakini waliopo ni 12 tu, ambao baadhi hawakubaliani na mawazo ya CCM lakini wanaambiwa mambo ni mazuri.
Ukawa walitoka kwa uhalali kabisa nami nawaunga mkono, sisi tuliobaki humu ndani tulikuja kwa makusudi ya kuangalia kinachoendelea na sasa tunaona mambo ni ovyoalisema.
Kwa upande mwingine alimlaumu Mwenyekiti wa Bunge
Maalumu Samuel Sitta kwamba amekuwa ni kinara wa kuvuruga kanuni kila
wakati na kutaka mambo yake mwenyewe.
Jumba ambaye ni mtaalamu wa sheria, aliwatupia
lawama pia viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba nao
wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwaweka Wazanzibar pamoja ili wajue
wanataka nini.
Kwa mujibu wa Juma, kila maeneo wanayojadili
wanafanya kazi hiyo kwa kuboresha maslahi ya CCM kwani wanawasaidia
kuwaandikia Ilani yao.
Alimtaka rais Jakaya Kikwete kukubaliana na maoni
ya watu mbalimbali kwamba bunge la Katiba lisitishwe mara moja kuliko
kuendelea kujadili misimamo mikali ya CCM.
0 comments:
Chapisha Maoni