Jumatano, Julai 30, 2014

WATOTO WAMNYONGA MWENZAO MWENYE MIAKA MITATU

Wakazi wa Kijiji cha Masusu, Kata ya Gisambalang wilayani Hanang’ katika Mkoa wa Manyara wamepatwa na mshtuko kutokana na tukio lenye utata la kuuawa mtoto Omary Hamis mwenye umri wa mitatu, kisha mwili wake kutundikwa juu ya mti.
Inadaiwa kuwa Omary aliuawa na watoto wenzake wawili ambao ni wakazi wa kijiji hicho kwa kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga na baadaye kuutundika mwili wake juu ya mti.
Watoto wanaodaiwa kufanya kitendo hicho (majina yao tunayahifadhi kwa sasa), mmoja ana umri wa miaka mitano na mwingine miaka saba  na wote wanashikiliwa na polisi katika Kituo cha Katesh, mkoani Manyara kwa uchunguzi zaidi.
Diwani wa Kata ya Gisambalang, Masala Bajuta alisema tukio hilo lilitokea Julai 26, mwaka huu saa 7 mchana na kwamba watoto wanaodaiwa kufanya kitendo hicho walikuwa wakichunga mifugo ndipo walipokutana na mtoto mwenzao.

0 comments:

Chapisha Maoni