WASICHANA saba wamepoteza maisha
wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha
kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.
Wasichana hao wamepoteza maisha kwa
nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa
wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana na waliwapigia simu ambapo
hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au
chupa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick
Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.
Mwananzila alikuwa amekwenda hospitalini
hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea
na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira hayo.
Alisema
serikali ya wilaya ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa roho za watu.
Mwananzila alisema kuwa binti mmoja
aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha
polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa
wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti
alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi waliwatia mbaroni watu hao. Mkuu
huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: “ni makosa kwa wasichana
kutoka nje baada ya kupigiwa …
kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike.
Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani
ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika. Alisema
suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza
na kuwataka wananchi wawe na subira.




0 comments:
Chapisha Maoni