WANANCHI wa Kigoma Kusini, wamesema wapo tayari kuunganishwa katika
kesi ya mbunge wao, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), wakidai kuwa sasa
kiburi cha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inabidi kifike
mwisho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara
iliyofanyika Kazuramimba, Basanza na Uvinza, wananchi hao walikataa
kuuliza maswali mengi badala yake wakitaka kuelekezwa utaratibu ili
waweze kuunganishwa kwenye kesi ya mbunge wao.
Mimi sina swali, ninataka kujua ni utaratibu gani unaweza kufanywa ili niweze kuunganishwa katika kesi inayomkabili mbunge wetu, kama mbunge wetu ameitwa tumbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya CCM ni dharau ya aina gani kwa sisi tuliomchagua, kwanini serikali ya CCM haijamkemea mwanasheria mkuu kutukejeli namna hii?
alisema mwananchi
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Luvakubandi, mkazi wa
Basanza.
Pamoja na mkazi huyo kuomba mwongozo huo, wazee kadhaa wa kata za
Kazuramimba na Uvinza nao walionekana kukerwa walipofika katika
mikutano ya Kafulila.
0 comments:
Chapisha Maoni