Kwa
sasa, yupo katika mwaka wa mwisho kabisa wa mkataba wake na anaweza
kulamimika kuhama baada ya kuanza mechi kumi (10) tu msimu uliomalizika.
Hivi karibuni, alijitokeza na kusema habari kuwa yupo mbioni kuamia
United ni za uongo kwani yeye bado ni mchezaji halali wa Arsenal na
akili yake kwa sasa imejidhatiti kuisaidia Ubelgiji huko Brazil. Lakini
sasa, amejitokeza tena akisema hajielewi itakuwaje!
Kwa kweli sijui nitachezea timu ipi (msimu ujao), Iwe Arsenal au mahala pengine. Akili yangu yote ilikuwa kwenye kombe la Dunia, lakini nitajua nikishazungumza na ArsenalVermaelen, akiliambia gazeti la London Evening Standard.




0 comments:
Chapisha Maoni