UHUSIANO wa kimapenzi unaimarishwa na mambo mengi kutegemeana na
wahusika wenyewe lakini haya matano (5) ambayo ni kusikilizana,
kuaminiana, kuheshimiana, kusaidiana, kushirikiana ni muhimu na
yakifuatwa vyema na pande zote mbili basi uhusiano wenu utakuwa mzuri na
wenye afya.
Mara zote tunapoanzisha uhusiano huwa hatuko wazi
kwa asilimia mia moja kusema tunataka nini kutoka katika uhusiano huo
mpya. Mara zote sisi wanawke ndio huwa tunakuwa na kimbelembele kujua
uhusiano tulionao unakwenda wapi katika kipindi kifupi, kwamba tunataka
kufahamu kama ni “ring au fling” lakini kwa vile wanaume tunaokuwa nao
kwenye uhusiano huwa hawataki kutukatisha tamaa au hanawana uhakika na
hisia zao juu yetu wanawake hulazimika kutudanganya na baadhi hulipa na
mahali kwa wazazi ili kutupa matumaini na at the end huwa hakuna ndoa.
Kwa wanawake inakuwa ngumu (baadhi hatujakuzwa hivyo) kuwaeleza wanaume
kuwa tunachotaka ni uhusiano usio makini (casual) ili kukidhi mahitaji
ya kifedha au kimwili na matokeo yake huwa tunatafuta njia za mkato ili
kuwaudhi wenza wetu hali itakayo wafanya wamalize uhusiano na sisi.
Wanaume hujikakamua na kusema wazi ikiwa hawako tayari kuwa nauhusiano
wa muda mrefu au hawako tayari kufunga ndoa kwa wakati huo na hivyo
huturahisishia wanawake(ambao sio ving’ang’anizi) kuelewa uhusiano wenu
utakwenda ama unakwenda wapi?.
Natambua kuwa kuna baadhi yetu
huwa na uhakika kuwa uhusiano wao ni “ndoa” baada ya miezi mitatu ya
kuwa pamoja na wengine huwachukua hadi miaka mitano kuwa tayari ama kuwa
na uhakika na wanachokitaka kutoka kwenye uhusiano, hii ni kutokana na
jinsi walivyokuzwa ama kushuhudia maisha mazuri au mabaya ya ndoa za
wazazi wao au ndugu wakaribu.
Swala muhumi ni kuchukulia mambo
taratibu na kutolazimisha (hasa kwa wanawake), ikiwa Mungu anataka kuwa
huyo uliye nae ndio awe mume/mke wako basi ndivyo itakavyokuwa hivyo
hali kadhalika ikiwa sio yeye hamtofika mbali hata kama utalazimisha
atafunga ndoa na wewe kukuridhisha tu au kuhofia umri au hata kuhofia
kudhaniwa Shoga na jamii inayomzunguuka.
Lakini ikumbukwe kuwa
sote wake kwa waume hatuna mioyo ya ujasili wa kufanya hivyo na baadhi
yetu huwa tunaonyesha kwa vitendo kuwa hatuko tayari kuuchukua uhusiano
tulionao kwenywe hatua ya juu zaidi na badala yake huwa tunafanya
vitendo bila kujitambua lakini vinaashiria wazi kabisa kuwa mtazamo wako
na wa mwenza wako kwenye uhusiano wenu ni tofauti japo kuwa mnapendana
kupita kiasi.
Vilevile kuna wakati unahisi ama unajua kabisa
kutoka moyoni mwako kuwa humpendi sana mpenzi wako kama ambavyo
ungependa kumpenda lakini unaendeleza uhusiano na yeye kwa kuhofia
kumuumiza au kumuonea huruma ingawaje mwishoni mmoja kati yenu ni lazima
atakumbana na ukweli na kuukubali ukweli huo kuwa hautakiwi.
Sasa, kuna vijimambo hujitokeza ndani yauhusiano ambavyo vitakufanya
utatambue kuwa mpenzi wako hayuko makini sana na wewe au kakuchoka ila
hajui jinsi yakutoka.
Uchelewaji: Mmeagana kukutana na wewe
umesubiri kwa takriban saa nzima, lakini anapofika ana-act kuchelewa
dakika tano tu na bila aibu wala huruma haombi msamaha kwa kukugandisha
vilevile hatokupa sababu ya msingi/maana (mwanamke kuchelewa kwenye
“date” ni muhimu na ni sehemu ya urembo ukiachilia mbali kujiandaa
kuku-impress wewe bali pia umuone wakati anaingia na kukufanya wewe
ujivunie kuwa na mrembo kama yeye).
Utani:Ni kitu kizuri na
husaidia kuwaweka karibu kimapenzi, lakini ikiwa mwenza wakoa nakutania
kuhusu mambo ambayo mnayafanya mkiwa wawili tu, au kasoro zako mbele ya
rafiki zake, ndugu zake nakukucheka huo hautakuwa utani bali
kukudhalilisha.
Kutotilia maanani: Mfano kuna swala muhimu
unataka mzungumze lakini yeye anapiga tarehe kila unapoomba muda na yeye
na siku akikubali kukaa chini ili mzungumze basi majibu yake yatakuwa
ndio au hapana, hatoi maelezo ya kutosha kuhusiana na issue unayomueleza
hasa ikiwa inahitaji maamuzi yenu kama wenza.
Kutojali: Wakati
wote wewe ni mtu wa kupiga simu kujua yuko wapi, ikiwa anaumwa au
anamatatizo kifedha wewe unakuwa pale kwa ajili yake lakini kibao
kikikugeukia humuoni na wala haonyeshi kujali kuwa unamatatizo na kwamba
anapaswa kuwa hapo kukupa moyo wa kukabiliana na yanayokukabili.
Sehemu ya mwisho ktk maisha yake: Kukatisha miadi na wewe kwa ajili ya
kuonana na rafiki zake, wakati wote wote wewe ni mkosaji mbele ya wazazi
wake na ndugu zake.
Kutengwa: Akitoka hatoki na wewe kwenda
matembezini, kila akichelewa kurudi basi alikuwa na rafiki ambae hupaswi
kumjua, hukutambulisha kwa jina lako badala ya “mpenzi wangu”
ikifuatiwa na jina lako.
Kutoheshimu ndugu familia yako: Sote
hatujakamilika, lakini ukikosea kidogo tu basi ukoo mzima utaunganishwa
kwenye kosa hilo Mf ndio maana mama’ko yuko hivi, umerithi kutoka kwa
baba yako, kwenu wote mko hivi au vile n.k.
0 comments:
Chapisha Maoni