Ujerumani imetwaa Kombe la Dunia kwa mara ya nne, baada ya kuibwaga
Argentina 1-0 katika fainali zilizomalizika hivi punde Rio de Jenariro,
Brazil. Washangiliaji waliomimika kwa maelfu kuangalia mechi hiyo ya
aina yake walikuwa wakiishangilia Argentina, huku zaidi ya raia 100,000
wa Argentina wakiripotiwa kumiminika nchini Brazil kupitia mpakani na
baharini, lakini hilo halikuwadumaza Wajerumani. Mario Götze
ndiye aliyeweka kimiani goli la kwanza na la pekee katika dakika 113 na
hivyo kuiandika nchi yake kwenye kitabu cha historia ya ushindi wa
Kombe la Dunia. Kwa mara ya kwanza Ujerumani ilishinda Kombe hilo mwaka
1954, kisha 1974 na 1990, wakati huo bado ikiwa imegawika kati ya
mashariki na magharibi. Ushindi wa mara hii ni wa kwanza tangu mashariki
na magharibi kurudi tena kuwa taifa moja la Jamhuri ya Shirikisho la
Ujerumani.
0 comments:
Chapisha Maoni