Zifuatazo ni tuzo mbalimbali zilizogawiwa kwa wachezaji mahili katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
adidas GOLDEN BALL
Hii ni tuzo ya mpira wa dhahabu ambayo hupewa mchezaji aliyefanya vyema
kwa ujumla katika mashindano, mshindi ni LIONEL MESSI wa Argentina.
adidas GOLDEN BOOT
Hii tuzo buenda kwa mchezaji aliyefunga goli nyingi katika mashindano,
amechuchuka JAMES RODRIGUEZ wa Colombia, ambaye ametia tia nyavu mara
sita (6) katika michuano hii.
adidas GOLDEN GLOVE
Hii tuzo
hupewa golinyanda bora kabisa kutoka michuanoni, ameichukua MANUEL
NEUER kutoka Ujerumani kutokana na udakaji bora kabisa kipindi chote cha
michuano.
Hyundai YOUNG PLAYER AWARD
Hii ni ya mchezaji
mwenye umri mdogo na aliyefanya vyema kabisa katika michuano. Amechukua
kiungo PAUL POGBA kutoka France kutokana na uchezaji mahiri kabisa
dimbani.
FIFA FAIR PLAY AWARD
Tuzo hii hupewa timu ambayo
imeonyesha kiwango cha juu kabisa cha nidhamu katika michuano, hata
hivyo, moja ya vigezo vikubwa ni kwamba lazima timu hiyo iwe imevuka
mzunguko wa kwanza na kuingia katika hatua ya mtoano ndipo itafikiriwa
kuwania tuzo hiyo. TEAM COLOMBIA, ndio wametwaa tuzo hii ikiwa
imeonyesha nidhamu thabiti safari hii, mara ya mwisho ilikuwa Spain
mwaka 2010.
0 comments:
Chapisha Maoni