Wananchi wa kijiji cha Mowo kata ya
Kimochi katika wilaya ya Moshi vijijini wameiomba serikali iwafikishie
umeme ili kuboresha huduma za kijamii zikiwemo za afya katika zahanati
yao ambayo sasa wameikamilisha.
Wananchi hao wametoa ombi hilo katika uzinduzi wa zahanati ya kijiji hicho iliyogharimu shs. 65mil/= zikiwemo nguvu na michango yao baada ya kusuasua kwa muda mrefu kutoka na migogoro. Wamesema, ingawa zahanati hiyo imekamilika lakini itakuwa haina thamani yoyote kwa kuwa dawa na huduma zingine za afya zinahitaji umeme wakati wote na kwamba kijiji hicho hakijawahi kuwa na umeme na huduma za afya. Wananchi hao wamesema, kukamilika kwa zahanati hiyo kumewasogezea karibu huduma za afya kwa kuwa walikuwa wanafiri umbali mrefu hadi moshi na wakati mwingine wagonjwa walikuwa wanafia njiana na wanawake kujifungulia njiani. Akizindua zahanati hiyo mbunge wa Moshi vijijini Dr Cril Chami amewataka wananchi wa kijiji hicho kudumisha ushirikiano kati yao katika kujiletea maendeleo badala ya kuzingatia malumbano na migogoro isiyo na tija na kuwataka waige mfano wa wananchi wa Uru na Kibosho.

0 comments:
Chapisha Maoni