Mkazi mmoja wa Mtaa wa Msamvu B mjini hapa, Rehema Juma
amekatwakatwa na wembe shavuni na mkononi kisha kuvuliwa nguo na kupigwa
na jirani yake akimtuhumiwa kutembea na mumewe.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita mnamo saa
11:00. Mwanamke huyo alidai kuwa kabla ya kujeruhiwa aliitwa na jirani
huyo na bila kujua alichoitiwa, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo
ambako alifungiwa ndani.
Alisema akiwa ndani jirani huyo alimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake na hata alipojaribu kukataa, alitishia kumuua.
Kwa kuhofia kuuawa niliona nikubali tuhuma hizo na aliniuliza ni mara ngapi nilifanya mapenzi na mume wake na kama nilikuwa napewa pesa, hivyo nilikiri kufanya mapenzi mara mbili na kwa mara ya kwanza alinipa Sh2,000 na mara ya pili alinipa Sh5, 000 na baada ya hapo aliniachia na nikarudi nyumbanialidai Rehema.
Rehema aliendelea kudai kuwa siku hiyo mnamo saa
11:00 jioni binti wa mwanamke huyo alifika tena nyumbani kwake na
kumwambia anaitwa tena na mama yake. Naye bila ya hofu alikwenda
nyumbani kwa mwanamke huyo na alipofika aliingizwa kwenye chumba kimoja
ambacho alikuwamo mume wa mwanamke huyo na kuanza kumpiga, akamvua nguo
na kumkatakata kwa kiwembe shavuni na mikononi.
Alidai kuwa baadaye mwanamke huyo alianza kumpiga
mume wake, lakini mwanaume huyo alichomoka na kukimbia na alipomkimbiza
ndipo yeye alipopata nafasi ya kutoka nje akiwa amebaki hana nguo huku
akichuruzika damu.
Aliporudi nyumbani kwake, Rehema alisema
aliongozana na mume wake Godfray Shichonge na ndugu zake wengine kwenda
polisi kutoa taarifa na baadaye walipewa PF3 kwenda kutibiwa.
Godfray Shichonge, ambaye ni mume wa Rehema alidai
kuwa tangu alipoanza kuishi na mkewe hajawahi kusikia taarifa zozote za
kufanya mapenzi nje ya ndoa yao na kuwa katika mtaa huo ni wageni na
hawana mazoea na mtu yeyote.
Alipoitwa nyumbani kwa mama huyu na kufanyiwa ukatili aliniacha nyumbani nikiwa nimepumzika na kabla ya kuondoka aliniaga na nikadhani kuwa ni masuala ya kawaida ya kina mama. Ghafla nilishtuka usingizini kutokana na kilio cha mke wangu aliyerudishwa nyumbani akiwa anavuja damu na akiwa amevuliwa nguo zotealisema Shichonge.
Alisema kitendo alichofanyiwa mke wake ni
udhalilishaji kwani hata kama mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu kufanya
mapenzi na mume wake alipaswa kufuata sheria na siyo kumjeruhi kwa
kumkata kwa viwembe na kumvua nguo.
Mjumbe wa mtaa huo, Dimoso Frances alisema baada
ya mwanamke huyo kumkatakata mwenzake kwa viwembe, alikwenda nyumbani
kwa mjumbe huyo na kuomba asamehewe kwani alifanya hivyo kutokana na
hasira.
Dimoso alidai kuwa kutokana na hali ya majeruhi
kuwa mbaya, hakuweza kutoa uamuzi wowote na hivyo aliamua kufuatilia
taarifa hizo polisi ambako aliambiwa kuwa tayari kesi ya kujeruhi
ilishafunguliwa kwa jalada namba MORO/IR/4009/2014.
0 comments:
Chapisha Maoni