Jumanne, Julai 08, 2014

ASKOFU MKUU ANGRIKANA ATOA TAMKO LA AMANI

Askofu mkuu wa kanisa la Angrikana nchini Mhashamu Jacobu Chimeledya amewatadhariwa waumini na watanzania kwa ujumla kutambua kuwa amani iliyopo inaweza kuendelea kumomonyoka na kuwa vurugu, kama hawatakuwa tayari kutoa taarifa kwa vyombo vya dora, juu ya watu wachache ambao wanajihusisha na utengenezaji wa milipuko.
Mhashamu Chimeledya ametoa kauri hiyo katika maubiri yake katika kanisa la angrikana mjini Tabora, katika maazimisho ya miaka 25 ya dayosisi ya Tabora, ambapo amesema kuwa, matukio  ya milipuko yanayojitokeza katika baadhi ya mikoa wahusika wamo katika jamii, ambayo kama ikishirikiana yanaweza kutolewa taarifa.  
Wakizungumzia misingi ya amani iliyopo ndani ya kanisa na taifa zima,  baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali wamesema kuwa, jamii ibadilike kwa kutambua amani ikitoweka waathirika wakubwa ni watanzania wote, na hakuna  pakukimbilia.  
Dayosisi ya Tabora imeazimisha miaka ishirini na tano kwa matukio mbalimbali ikiwemo shughuli za kimaendeleo kama kuanzishwa kwa shule za sekondari, na vituo vya afya, likiwa na lengo la kutoa mchango kwa serikali katika huduma za kijamii katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

0 comments:

Chapisha Maoni