Kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 31, amekataa kujiunga na
Manchester United (Daily Star), kiungo wa Everton Ross Barkley, 20,
anatazamwa na Man City kuziba nafasi ya Yaya Toure, iwapo atalazimisha
uhamisho na kuondoka Etihad (Daily Mail), beki wa kulia wa Arsenal Carl
Jenkinson, 22, anasakwa na West Ham (Sun), Sunderland wamemuulizia winga
wa Atletico Madrid Cristian Rodriguez, 28, (Daily Mail) mshambuliaji wa
zamani wa Man City Mario Balotelli, 23, ameonesha
dalili kubwa za kutaka kuhamia Arsenal, baada ya kupiga picha mbele ya
nembo ya Arsenal (Daily Star), meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
anataka kuendelea kununua wachezaji licha ya matumizi ya Liverpool
kuonekana huenda yakazidi pauni milioni 100, kwa mara ya kwanza katika
historia ya klabu hiyo (Liverpool Echo), Liverpool imeulizia kama
wanaweza kumchukua winga wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali (Daily
Express), Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira anafikiria kuzikataa
Arsenal na Chelsea na kusalia na mabingwa wa Ulaya (Daily Express), boss
wa West Brom Alan Irvine amesema hatua ya Manchester United kumnunua
Luke Shaw kwa pauni milioni 30 imesababisha bei ya mabeki kupanda (Daily
Mirror), meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal anataka
kumteua Paul Scholes kuwa mmoja wa wasaidizi wake (Manchester Evening
News), Van Gaal pia ametaka uwanja wa mazoezi wa Carrington kufanyiwa
mabadiliko kwa sasaba "una upepo mkali" (Daily Mail), kiungo wa Arsenal,
Jack Wilshere amerejea mapema na kuanza mazoezi baada ya kushutumiwa
kwa kuonekana akivuta sigara mjini Las Vegas (Daily Telegraph), na
hatimaye winga kutoka Ufaransa Hatem Ben Arfa ameingia katika mzozo na
klabu yake ya Newcastle kuhusiana na "unene" wake, yeye anadai amejenga
misuli na kusema ni makosa kwa Newcastle kumpiga faini kwa kudai ni
"manyama uzembe" (Daily Mirror).
0 comments:
Chapisha Maoni