Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi
kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania
haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa
Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria
ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
Wanakijiji hao zamani walikuwa
wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi
wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete
Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza
leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi
kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.
Mwandishi wa BBC Leonard Mubali, anaandaa
taarifa hiyo huko wilayani Makete na baadaye utaweza kuisikiliza katika
redio na hapa kwenye mtandao.
Lakini kwa sasa tunaulijza je ni ni sawa kwa
Bangi kuhalalishwa kama chakula nchini Tanzania?
0 comments:
Chapisha Maoni