Arsenal wamepata matumaini zaidi ya kumsajili Sami Khedira, 27, baada ya
kiungo huyo kukataa kusaini mkataba mpya na Real Madrid (Daily Star),
Arsenal pia wapo katika mazungumzo ya kumsajili Loic Remy kwa pauni
milioni 8 kutoka QPR iliyopanda daraja (Independent), hata hivyo
mazungumzo kati ya Arsenal na Remy yanadaiwa kuvunjika baada ya Remy
kutokubali maslahi binafsi, huku Newcastle na Tottenham wakitaka
kumchukua (Daily Mail), Chelsea wanataka pauni milioni
8 kwa ajili ya beki Ryan Bertrand, 24, ambaye ananyatiwa na Liverpool
na Tottenham (Daily Express), mshambuliaji wa zamani wa Arsenal
Marouanne Chamakh, 30, amekubali mkataba wa miaka miwili kusalia Crystal
Palace, huku akikubali kupunguziwa mshahara kiwango kikubwa (Guardian),
Liverpool wameingia kwenye mbio sawa na Tottenham za kumsajili Wilfried
Bony, 25, ambaye Swansea wanamuuza kwa pauni milioni 20 (Talksport),
Lazio wanaamini wana kipaumbele zaidi kumsajili Stefan De Vrij, 22,
kutoka Feyenoord, ambaye anasakwa pia na Manchester United (Daily
Express), kiungo wa Spain Mikel Arteta, 32, hana nia ya kuhama Arsenal
kwa mujibu wa wakala wake Inaki Ibanez (Times), Arsenal wana matumaini
ya kukamilisha usajili wa Javi Manquillo kutoka Spain na Mathieu
Debuchy, kuziba nafasi za Bacary Sagna na Carl Jenkinson (Daily Mail),
Everton huenda wakamsajili Muhamed Besic, 21, raia wa Bosnia Herzegovina
kwa euro milioni tano (Daily Mirror), kiungo wa Juventus amezua gumzo
zaidi la kuhamia Chelsea baada ya kuonekana katika mitaa ya Stamford
Bridge (Daily Mail), Manchester United huenda wakamfuatilia Ben Davies
kuziba nafasi ya Patrice Evra (Daily Mail), Chelsea wamejiunga na
Arsenal na Liverpool kumwania mshambuliaji wa Real Sociedad Antoine
Griezman, 23 aliyekataa mkataba mpya (Daily Express), mshambuliaji wa
Real Madrid Alvaro Morata, anatazamiwa kwenda Juventus kwa pauni
milioni 17.5. Real Madrid watakuwa na uwezo wa kumnunua tena baada ya
mwaka mmoja kwa pauni milioni 23.8 (Daily Mail). Hizo ndio tetesi za
leo, share na wapenda soka wote. Nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!




0 comments:
Chapisha Maoni