Jumapili, Julai 13, 2014

TETESI MPYA ZA USAJILI ULAYA NA HISPANIA

*Di Maria 'kuitosa' Man U
*Liverpool kusajili wengine SITA
*Suarez kukatwa mshahara akirudia 'mchezo wake'
Juventus wanajipanga kutoa pauni milioni 20 kumchukua Paulinho, 25, kutoka Tottenham, hatua hiyo huenda ikatoa mwanya kwa Manchester United kumchukua Arturo Vidal, 27 (Sunday Telegraph), winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 27, huenda akakataa kwenda Manchester United licha ya kupewa mshahara wa 150,000 kwa wiki (Daily Express), mshambuliaji wa Ecuador Enner Valencia, 25, amewasili London kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham kutoka klabu ya Pachuca ya Mexico (The Sun on Sunday), Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Eliaquim Mangala, ambaye Manuel Pellegrini anaamini atacheza vyema na Vincent Kompany (Mail on Sunday), boss mpya wa Manchester United Louis van Gaal, ambaye huenda akaingia rasmi Old Trafford siku ya Alhamisi, anatarajia kuwasajili Mats Hummels na Marco Reus (Sunday Express), Van Gaal, 62, pia amemwambia winga Arjen Robben kuwa anakaribishwa Old Trafford (Sunday Telegraph), Liverpool wanajiandaa kutoa pauni milioni 26 kumsajili Romelu Lukaku, 21, kutoka Chelsea (Caughtoffside.com), Newcastle imewasiliana na Monaco kujaribu kumsajili mshambuliaji Emmanuel Reviere, 24 (Sunday Mirror), AC Milan wamesema hawatomsajili tena beki Sime Vrsaljiko ambaye anasakwa na Arsenal (Talksport), Dynamo Moscow wanataka kumchukua Wilfired Zaha, 21, kutoka Manchester United baada ya kumchukua Alex Buttner (Sun on Sunday), beki wa kati wa Roma Mehdi Benatia anataka kuhamia Chelsea (Gazetta dello Sport), Barcelona wanamtazama kwa karibu beki wa Tottenham Jan Vertonghen. Barca pia wanamfuatilia Mats Hummels wa Borussia Dortmund (Mundo Deportivo), mshambuliaji wa Manchester United Bebe amefikia makubaliano na Benfica ya uhamisho wa kudumu. Klabu hizo mbili bado hazijakubaliana bado kuhusu ada (A Bola), Angel Di Maria angependa kwenda Paris Saint-Germain badala ya Manchester United ambayo haichezi Champions League msimu ujao (Sunday Times), boss wa Chelsea huenda akamchukua Javier Pastore kutoka PSG kwa pauni milioni 25 iwapo mabingwa hao wa Ufaransa watamchukua Angel Di Maria (Daily Express), licha ya kununua wachezaji watatu mpaka sasa, boss wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kununua wachezaji wengine sita. Rodgers ameambiwa anaweza kutumia kitita chote cha kumuuza Luis Siarez, na henda akatumia hadi pauni milioni 135 (Sunday People), na Luis Suarez huenda akakatwa pauni milioni 3 katika mshahara wake wa pauni milioni 10 kwa mwaka ikiwa atamng'ata mchezaji mwingine akiwa Barcelona (Sunday People). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

0 comments:

Chapisha Maoni