KUNA watu wajanja aisee. Unajua ni nini, kipa Ivo Mapunda wakati
wenzake wa Simba wakimaliza mazoezi na kurejea makwao yeye wala haendi
nyumbani, huwa anabaki uwanjani na kuendelea na mazoezi na kipa mkongwe,
Peter Manyika.
Mtandao wa Fichuo Tz Blog umemshuhudia Ivo akikomaa na Manyika
ambaye ni kipa wa zamani wa Yanga na baba mzazi wa Manyika Peter, kipa
chipukizi aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni anayechezea Simba B.
Akizungumza katika Uwanja wa Karume anapofanyia
mazoezi hayo, Ivo alisema hizo ni jitihada zake za kujiweka fiti kwa
ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mazoezi haya yananipa uimara zaidi na wepesi hasa miguuni na tumboni, nitaendelea kufanya mazoezi haya kila ninapopata muda wa ziada hasa tunapokuwa mapumzikoalisema Ivo.
Alisema mazoezi hayo yamemsaidia kupunguza uzito kwani alifikia kilogramu 85 na kumfanya ajisikie mzito.
alisema.Sijapima bado kujua nimepunguza ngapi, lakini kwa sasa ninajisikia mwepesi
0 comments:
Chapisha Maoni