Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari
kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo
ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia
utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati
wa siku kuu ya Eid ul Fitr.
Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
Mwandishi
wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu
kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi
yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi
katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa
anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi
kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa
hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.
0 comments:
Chapisha Maoni