Jumatatu, Julai 28, 2014

LIBERIA YAFUNGA MIPAKA KWA HOFU YA EBOLA

Serikali ya Liberia imefunga vituo vyake vya mpakani kwa kuhofia kuenea virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola nchini humo. Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia ametaja kasi ya kuenea virusi vya ugonjwa huo kuwa ni changamoto kubwa ya kiafya na kuongeza kuwa, serikali itafunga vivuko vyote vya kuingia nchini humo isipokuwa vivuko vikuu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Monrovia itaanzisha huduma za kugundua maambukizi ya ugongwa huo hatari katika vituo hivyo vikuu sanjari na kuchukua hatua kali za kiafya. Mbali na hapo Liberia imekwishatekeleza baadhi ya hatua katika kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo ikiwemo kuzuia aina zote za mikusanyiko ya watu kama maandamano na makongamano ya kijamii. Hata hivyo na licha ya juhudi zote hizo, bado ugonjwa huo umeendelea kusambaa kila uchao ndani ya nchi hiyo suala ambalo limeibua hali ya wasiwasi kwa serikali. Ripoti zinasema hadi sasa zaidi ya watu 600 wamepoteza maisha yao tangu kulipoibuka ugonjwa huo katika eneo la magharibi mwa Afrika miezi michache iliyopita.

0 comments:

Chapisha Maoni